Hatua hiyo ni sehemu ya mikakati endelevu ya TBS ya kulinda afya na usalama wa wananchi kwa kuondoa sokoni bidhaa zisizo na viwango.
Aidha, inalenga kujenga imani ya watumiaji kwa ubora wa bidhaa zinazopatikana sokoni na kuhakikisha soko linakuwa salama.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa udhibiti ubora Mwandamizi kwa niaba ya Meneja wa TBS Kanda ya Kaskazini, Bw. Edward Mwamilawa, alisema operesheni za ukaguzi zinaendeleakufanyika mara kwa mara katika maduka na maghala.
“Tutaendelea na ukaguzi na kuondoa sokoni bidhaa zisizokidhi viwango alisema Bw. Mwamilawa.
Aliwataka wananchi kuwa makini wanaponunua au kuagiza bidhaa kwa kuzingatia tarehe za mwisho wa matumizi, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa umma katika kubaini na kuripoti bidhaa hatarishi.
Kwa upande wake, Afisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Bi. Sauda Leveri, alisema ukaguzi utaendelea sambamba na uthibitishaji wa vibali vya TBS katika maeneo ya biashara.
“Wananchi wanapaswa kuwa waangalifu wanapotumia bidhaa, hasa za vyakula, ili kuepuka madhara ya kiafya,” alisema Bi. Leveri.




No comments:
Post a Comment