Bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na vyakula ambavyo havijasajiliwa, vipodozi vyenye viambata hatarishi kwa afya, bidhaa zilizokwisha muda wake wa matumizi (expired) pamoja na nguo za ndani za mitumba.
Hatua hiyo ni sehemu ya mikakati endelevu ya TBS ya kulinda afya na usalama wa wananchi kwa kuondoa sokoni bidhaa zisizokidhi viwango vilivyowekwa.
Aidha, hatua hiyo inalenga kujenga imani ya walaji juu ya ubora wa bidhaa zinazopatikana sokoni na kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa salama, lenye ushindani na mchango chanya katika maendeleo ya taifa.



No comments:
Post a Comment