Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum na Mwakilishi wa Kudumu wa Liberia katika IMO, Balozi Wilmot Kpadeh wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi ya Libaria kwa katika masuala ya usafirishaji kwa njia ya Bahari ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum na Mwakilishi wa Kudumu wa Liberia katika IMO, Balozi Wilmot Kpadeh wakionesha hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi ya Libaria kwa katika masuala ya usafirishaji kwa njia ya Bahari ,jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
TANZANIA imepiga hatua kubwa katika safari ya kuwa kitovu cha usafiri wa majini katika ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kusaini Hati ya Makubaliano (MOU) ya kihistoria na nchi ya Liberia, yenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika usajili wa meli, mafunzo kwa mabaharia na usimamizi wa sekta ya bahari.
Makubaliano hayo yalisainiwa jana katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa juu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Tanzania (TASAC) pamoja na Mamlaka ya Bahari Liberia (LiMA) nchini Liberia, mashirikiano hayo yakitajwa kuwa hatua muhimu katika kukuza uchumi wa buluu barani Afrika.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mohamed Salum, alisema makubaliano hayo si ya ishara tu bali ni mfumo rasmi wa ushirikiano wa vitendo.
“Huu ni mfumo uliopangwa kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa sekta ya bahari, kujenga uwezo wa rasilimali watu na kuweka kanuni zinazoendana na mwelekeo wa dunia,” alisema.
Amesema kuwa uzoefu wa Liberia kama kinara wa Kimataifa katika usajili wa meli na usimamizi wa viwango vya kimataifa utatoa fursa ya kipekee kwa Tanzania kuimarisha daftari lake la kimataifa la usajili wa meli pamoja na kuongeza ubora wa wataalamu wake wa baharini.
Amesema nchi ya Liberia ina uzoefu wa miongo kadhaa katika usafirishaji wa kimataifa na ushiriki wake katika International Maritime Organization (IMO).
Kupitia makubaliano hayo TASAC watanufaika na programu za kubadilishana uzoefu, mafunzo ya kitaalamu pamoja na fursa za kupata vyeti vinavyotambulika kimataifa, vitakavyowawezesha kufanya kazi katika meli zilizosajiliwa chini ya bendera ya Liberia.
Mwakilishi wa Kudumu wa Liberia katika IMO, Wilmot Kpadeh, alisema makubaliano hayo ni hatua ya kihistoria itakayojenga urithi wa kudumu kwa mataifa hayo mawili.
“MOU hii inaweka msingi wa urithi ambao vizazi vijavyo vitauthamini. Afrika inachangia asilimia nne tu ya mabaharia milioni 1.9 duniani licha ya kuwa na ukanda mrefu wa pwani. Kupitia ushirikiano huu, tunaweza kufundisha, kuthibitisha na kuwawezesha wataalamu wapya wa bahari kutoka Afrika,” alisema.
Aidha, ushirikiano huo utaipa Tanzania nafasi ya kunufaika na uzoefu wa Liberia katika ushiriki wa shughuli za IMO. Ingawa Tanzania si mjumbe wa Baraza la IMO, makubaliano hayo yataiwezesha kushiriki katika uwasilishaji wa hoja na mijadala ya sera katika ngazi ya kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum (kushoto)akimpa zawadi Mwakilishi wa Kudumu wa Liberia katika IMO, Balozi Wilmot Kpadeh mara baada ya kusaini hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi ya Libaria kwa katika masuala ya usafirishaji kwa njia ya Bahari ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubaliano ya Ushiriakiano na Mamlaka ya Bahari ya nchini Liberia (LiMA) katika hafla uliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha za mukundi mbalimbali mara baada ya kuhitimisha utiaji saini ya hati ya makubaliano kati ya Tanzania na Liberia katika eneo la usafirishaji kwa njia ya Bahari jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano na Mamlaka ya Bahari ya nchini Liberia (LiMA) katika hafla uliyofanyika jijini Dar es Salaam.


.jpeg)

.jpeg)



No comments:
Post a Comment