Serikali imejidhatiti katika kuboresha huduma za mawasiliano na kuleta mageuzi ya teknolojia ya kidigital ili kuboresha utoaji wa huduma, kuimarisha utawala bora na ukuaji wa uchumi huku ikipanua wigo wa ushiriki wa wananchi katika shuguli za kimaendeleo.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari Mh Angellah Kairuki wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa maduka 31 ya @airtel_tanzania, ambapo amesema serikali inashirikiana na wadau mbalimbali kama Airtel Tanzania katika kufanya uwekezaji wa miundombinu bora na ya kisasa ya mawasiliano ili kutanua wigo wa huduma kwa wananchi.
Aidha Waziri Kairuki amesema kama wizara wanatambua umuhimu wa maduka hayo na kwamba hatua hiyo itasaidia si tu kufikisha huduma bali itafungua milango ya fursa za ajira kwa watanzania hususani vijana,
Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka @airtel_tanzania Adriana Lyamba amesema @airtel_tanzania imezindua maduka hayo kwakuwa inawathamini wateja wake na inataka kuwafikishia huduma kwa urahisi.
Maduka hayo yaliyozinduliwa leo maduka manne yapo jijini Dodoma,na maduka 27 yapo mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha


No comments:
Post a Comment