HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 3, 2026

FCC YAWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI

Tume ya Ushindani (FCC) imeweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa wakati, kupitia matumizi ya mifumo ya kisasa katika utekelezaji wa majukumu yake.

Akizungumza wakati wa kikao kazi na watumishi wa Tume hiyo kwa lengo la kupanga mikakati ya utekelezaji wa majukumu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa, amesema hatua hizo zinalenga kuongeza ufanisi wa huduma na kuwahudumia wananchi kwa viwango vya juu vya ubora.

Amesema FCC inaendelea kutekeleza dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha mazingira ya biashara nchini yanaboreshwa na kuwashirikisha wafanyabiashara kupitia mifumo rafiki na yenye ufanisi.

Ngasongwa amesema kuwa katika kipindi cha siku 100 za uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, FCC imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kusogeza huduma karibu na wananchi, ikiwemo kuanzisha Ofisi ya FCC Mkoa wa Tanga na Mipakani ili kuongeza wigo wa utoaji huduma na kuwafikia wananchi wengi zaidi, hususan wale waliopo maeneo ya pembezoni mwa nchi. 

Ameongeza kuwa FCC imeendelea kudumisha cheti hicho cha ubora kutokana na jitihada zake katika utoaji wa huduma kwa wananchi na wadau wa biashara kwa weledi na uwazi.

“Tuko hapa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kwa viwango vya ubora vinavyotambulika kimataifa, niwapongeze kwa kuendelea kushikilia Cheti cha Ithibati ya Ubora ISO 9001:2015,” amesema Ngasongwa.

Vilevile watumishi walipata nafasi ya kupitishwa na kujadili tathmini ya rasimu ya Mpango Mkakati Mpya wa Tume wa miaka mitano (Strategic Plan) 2026/27-2030/31 unaoakisi utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050. 

FCC ina utamaduni shirikishi katika kujadili mambo yahusuyo taasisi, ambapo watumishi wote kupitia ngazi mbalimbali hushirikishwa kwa ustawi wa taasisi. 

Kikao hicho kimefanyika Februari 02,2026 katika ukumbi wa Hoteli ya Tiffany Diamond, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa akizungumza na watumishi wa FCC (hawapo pichani) katika kikao kazi na watumishi wa Tume, kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tiffany Diamond, Jijini Dar es Salaam Februari 02,2026.
Bw. Shalua Magandi, Mkurugenzi wa Huduma Saidizi akichangia mada wakati wa kikao kazi na watumishi wa Tume, kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tiffany Diamond, Jijini Dar es Salaam Februari 02,2026.Mwenyekiti wa Tughe Tawi la FCC, Bw. Emmanuel Ndyetabula akifuatilia kikao kazi cha Kaimu Mkurugenzi Mkuu na watumishi wa Tume, kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tiffany Diamond, Jijini Dar es Salaam Februari 02,2026.


Sehemu ya watumishi.




Picha za pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad