Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogoro amesema Tume ya Ushindani (FCC) kuongeza watumishi kutokana na majukumu yake kuwa makubwa ikiwemo kuongezeka kwa shehena katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mpogoro ameyasema hayo wakati akiwa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila kufungua Semina ya Wahariri iliyoandaliwa na Tume ya Ushindani (FCC) jijini Dar es Salaam .
Amesema FCC chombo ambacho kinaangalia uchumi wa soko pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora.
Mpogoro amesema kuwa zamani kulikuwa na kuwepo kwa luninga zisizo na ubora lakini FCC imefanya kazi yake.
Aidha amesema kuwa FCC Wahariri ni njia muhimu katika kuwa daraja la kufanikisha kutoa elimu kwa wananchi juu majukumu ya FCC.
Mpogoro amesema kuwa FCC Wilaya ya Ilala itaendelea kushirikiana na FCC kwani Ilala ndio lango la bidhaa za nje na ndani katika kuendelea kuwepo kwa ushindani wa soko.
Amesema kuwa semina hiyo wahariri wapitishwa katika sheria ya ushindani 2003 ili wajue majukumu yake pamoja na sheria wanayotaka kupeleka bungeni ya Uhafueni.
Khadija amesema kuwa FCC inafanya kazi na taasisi zingine za kiudhibiti ikiwa ni kuhakikisha bidhaa zinaendelea kuwa bora na zenye ushindani wa soko .
Amesema kuwa FCC haiko tayari kuona soko linapangwa na kufanya wananchi waweze kuumia katika upatikanaji bidhaa.
Amesema Serikali ya Awamu Sita imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji hivyo ni wajibu FCC kuona maono ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)Bakari Kimwanga amesema kuwa semina hiyo ni muhimu sana katika kuendelea kuilinda nchi yetu katika kuendelea kuwepo kwa soko la ushindani.
Bakari amesema kuwa FCC imefanya jambo la msingi katika kushirikisha wahariri katika kuendelea kutoa elimu ya ushindani wa soko nchini.

.jpeg)
No comments:
Post a Comment