Mkazi wa Katoro, Baraka Malima, amejishindia pikipiki aina ya TVS baada ya kuibuka mshindi katika promosheni ya Airtel Tanzania ijulikanayo kama Airtel Mwaka Umenyooka.
Baraka alishinda zawadi hiyo kufuatia kufanya muamala wa kumtumia dada yake kiasi cha shilingi elfu ishirini na tano (25,000/-) kwa ajili ya matumizi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Malima alisema alishangaa kupokea taarifa za ushindi wake, akieleza kuwa kitendo cha kumtumia dada yake fedha kiligeuka kuwa baraka kwake.
“Nimetuma pesa kwa dada yangu kama msaada wa kawaida wa matumizi, lakini baadaye nikapokea taarifa kuwa nimejishindia pikipiki. Ni jambo la kushukuru sana,” alisema Malima.
Malima, ambaye anajishughulisha na shughuli za uchimbaji madini, amesema ataitumia pikipiki hiyo kurahisisha usafiri na shughuli zake za kila siku migodini.
Akikabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Airtel Mkoa wa Geita, Joseph Mushi, alisema promosheni ya Airtel Mwaka Umenyooka inaendelea na inatoa fursa kwa wateja kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo gari aina ya Mazda CX-5, bajaji, pikipiki, televisheni pamoja na fedha taslimu.
Airtel imewahimiza wateja wake kuendelea kutumia huduma zake ili kupata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali zinazotolewa kupitia kampeni hiyo.






No comments:
Post a Comment