
Nahodha Grayson Marwa ni Mkaguzi Mwandamizi wa Meli Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi na majaribio ya Boti ya Utafutaji na Uokoaji Mkoani Kigoma
Maafisa wa TASAC na Wazabuni wa Boti ya Utafutaji na Uokoji wakiwa ndani ya Boti mara baada ya kuifanyia majaribio Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.
TASAC YAPOKEA BOTI YA UTAFUTAJI NA UOKOJI KIGOMA
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa vyombo vya utafutaji na uokozi kwa watumiaji wa vyombo usafiri ni kipaumbele katika kuimarisha usalama wa usafiri majini katika Ziwa Tanganyika.
Hayo ameyasema Nahodha Gryson Marwa, Afisa Mwandamizi wa Ukaguzi na Usajili wa Meli kutoka (TASAC) wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukaguzi, majaribio na mapokezi rasmi ya boti ya utafutaji na uokoaji (SAR – TASAC II) katika Bandari ya Kigoma.
Marwa ameongeza kuwa TASAC inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha ununuzi wa boti tano za utafutaji na uokoaji ikiwemo na
Mkoa wa Kigoma kupata boti moja katika kuongeza ufanisi wa utoaji msaada pale dharura za majini zinapotokea.
Marwa amesema boti hiyo imepokelewa na kukaguliwa na kuona imekidhi vigezo vilivyokuwa vinatakiwa.
Hata hivyo amesema kuwa boti hiyo ilianza kukaguliwa tangu ilipoanza kutengenezwa, na majaribio ni uthibitisho wa kiufundi kabla ya kuanza kutumika rasmi katika maji ya Ziwa Tanganyika.
“Mwendelezo huu ni dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza kwa vitendo maombi ya mahitaji ya wananchi.
Amesema boti hiyo itaongeza usalama na kupunguza madhara ya ajali ya usafiri majini kwa kuhakikisha msaada unapatikana kwa haraka.
Kwa upande wake, Nahodha Adam Mamiro, Afisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Kigoma, amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Boti ya Utafuataji na Uokoaji kwa Mkoa wa Kigoma katika kurahisisha na kuharakisha operesheni za utafutaji na uokoaji kwa wavuvi na wasafiri wa Ziwa Tanganyika.
Nahodha Mamiro amesema Boti hiyo itahudumia maeneo ya jirani ya Katavi na Rukwa huku watumiaji wa vyombo vya majini wanapaswa kuendelea kuzingatia matumizi ya vifaa vya uokozi kama sehemu ya tahadhari binafsi.
Mvuvi wa mwalo wa Kigodeko Choba Aiseni wameishukuru Serikali kwa uwekezaji huo wakisema hapo awali walikumbana na changamoto kubwa ya kuokolewa kwa wakati, hasa wakati wa upepo mkali wa Kaskazi, Nyamori na Sabasaba.
“Kwa kupata boti hii tumefurahi sana kuona boti hii, sasa tuna uhakika kuwa msaada utapatikana kwa haraka tunapokumbwa na dharura majini,” amesema Aiseni.
Matukio mbalimbali ya majaribio ya Boti ya Utafutaji na Ukoaji Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.




.jpeg)
.jpeg)

No comments:
Post a Comment