Na Saidi Lufune, Dodoma
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb.), amesema kuwa Serikali inatarajia kulipa Shilingi Milioni 524.1 kwa wananchi 1,603 wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mkoani Mara kwa ajili ya malipo ya kifuta jasho na machozi kufuatia athari zinazotokana na wanyamapori wakali na waharibifu.
Mhe. Chande amebainisha hayo Bungeni jijini Dodoma akijibu swali la Mhe. Boniphace Mwita Getere (Mb), aliyetaka kufahamu, ni lini wananchi walioharibiwa mazao yao na tembo katika vijiji 9 vya Jimbo la Bunda vijijini watalipwa kifuta jasho.
“Kwa sasa Wizara inakamilisha taratibu za malipo hayo ili wananchi husika walipwe stahiki yao kwa mujibu wa Kanuni kupitia mfumo wa kieletroniki wa Problem Animal Information System (PAIS). Sambamba na mfumo huu mpya, kwa sasa Serikali itaendelea kulipa wananchi ambao hawana akaunti namba za benki au namba za simu kwa kutumia utaratibu wa awali ambapo wataalam hufika uwandani kufanya malipo hayo.” Alisema Mhe. Chande
Awali Mhe. Chande alieleza kuwa, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara ililipa kifuta jasho na machozi jumla ya Shilingi 312,360,000/= kwa wananchi 1,115 wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.



.jpeg)

.jpeg)

No comments:
Post a Comment