HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 24, 2026

Meridianbet Yahakikisha Mazingira Ni Salama Mbezi Juu

 

MERIDIANBET imeendelea kuthibitisha kuwa mchango wake hauishii kwenye burudani ya michezo ya kubashiri pekee, bali unagusa moja kwa moja maisha ya wananchi. Kupitia mkakati wake wa uwajibikaji kwa jamii (CSR), kampuni hiyo imeshiriki kikamilifu katika zoezi la usafi wa mazingira Kata ya Mbezi Juu, ikionesha dhamira ya kweli ya kushiriki maendeleo ya kijamii na kiafya ya wananchi.

Katika kuimarisha mapambano dhidi ya uchafu na magonjwa yanayotokana na mazingira yasiyo safi, Meridianbet ilishiriki usafi pamoja na kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi ikiwemo mifagio imara, mafyekeo, koleo, glovu, mifuko ya taka pamoja na viatu maalum vya kazi. Msaada huu ulilenga kuendeleza zoezi la usafi kwa muda mrefu na kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni, mwakilishi wa Meridianbet Nancy Ingram alieleza kuwa mazingira safi ni nguzo muhimu ya kuzuia magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, homa ya matumbo na maambukizi mengine yanayohusiana na uchafu. Alisisitiza kuwa Meridianbet inaamini kuwa jamii yenye afya bora ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Diwani wa Kata ya Mbezi Juu aliipongeza Meridianbet kwa kuonesha ushirikiano wa dhati na serikali za mitaa katika kulinda mazingira. Alieleza kuwa mchango wa sekta binafsi katika shughuli za kijamii ni kichocheo muhimu cha uwajibikaji wa pamoja, kwani huongeza hamasa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda afya zao na mazingira yanayowazunguka.

Kupitia tukio hili, Meridianbet imeweka wazi kuwa itaendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii yenye athari chanya kwa maisha ya wananchi. Kampuni hiyo imesisitiza kuwa usafi wa mazingira ni wajibu wa kila mdau, na itaendelea kushirikiana na jamii, viongozi na taasisi mbalimbali kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad