HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 24, 2026

GS1 TANZANIA YAIMARISHA UTAMBULISHO WA BIDHAA, YACHOCHEA USHINDANI NA MAGEUZI YA KIDIJITALI

 

Mkurugenzi wa Utafiti Viwanda TRIDO na Muwakilishi wa Mgeni rasmic, Humfrey Ndosi, katikati akizungumza wakati wa uzinduzi wa miaka 15 ya Gs1 Tanzania, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Jamuari 24, 2026.

Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Utambulisho wa Bidhaa Tanzania (GS1 Tanzania) imeadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, hatua iliyoelezwa kuwa na mchango mkubwa katika kukuza biashara, viwanda na ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Januari 26, 2026 jijini Dar es Salaam yakihusisha wadau wa sekta binafsi, taasisi za umma na wataalamu wa teknolojia ya biashara.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Fatma Kange, amesema GS1 imepitia safari ndefu ya mabadiliko tangu ilipoanzishwa, ikianza na shughuli za siku moja na sasa kuelekea mifumo ya kisasa inayohusisha teknolojia za kidijitali.

Amesema GS1 Tanzania inaendelea kubadilika kulingana na mahitaji ya soko na mabadiliko ya teknolojia, huku maandalizi ya maadhimisho makubwa yakipangwa kufanyika rasmi Septemba mwaka huu.

“Kama taasisi, tunajiuliza tunatoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi. Teknolojia zinabadilika kwa kasi, na GS1 Tanzania ina wajibu wa kuhakikisha wanachama wake hawabaki nyuma,” amesema Fatma,

Pia amebainisha kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuwasaidia wazalishaji na wafanyabiashara kutambulisha bidhaa zao kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utafiti Viwanda TRIDO na Muwakilishi wa Mgeni rasmic, Humfrey Ndosi, amesema GS1 imekuwa chombo muhimu katika kusaidia viwanda vya ndani kuboresha ushindani wa bidhaa zao, hasa kwa kuwezesha utambulisho unaokubalika kimataifa.

Ameeleza kuwa kabla ya uwepo wa GS1, wazalishaji wengi walikumbana na changamoto za kuingiza bidhaa zao sokoni, hali iliyowalazimu wengine kutegemea masoko ya nje.

Licha ya hayo aliwasilisha salamu za wizara na kuipongeza GS1 Tanzania kwa mchango wake katika kukuza sekta binafsi.

Amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi kama GS1 katika kujenga mazingira wezeshi ya biashara na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi.

Ameeleza kuwa mafanikio ya GS1 Tanzania yametokana na ushirikiano mpana kati ya serikali na sekta binafsi, ikihusisha taasisi mbalimbali zikiwemo TRIDO, TBS, BRELA, SIDO, TPSF, ZNCC, TCCIA, CTI, TAHA pamoja na vyama vya wazalishaji wa mazao na viungo.

Katika maadhimisho hayo, GS1 Tanzania imetangaza kuendelea na mabadiliko ya kidijitali, ikiwemo uzinduzi wa mfumo wa 2D migration, unaolenga kuboresha zaidi utambulisho wa bidhaa za Tanzania na kuongeza ufanisi katika minyororo ya thamani ya biashara.

Ufunguzi wa Maadhimisho hayo yametoa wito kwa Watanzania kujiamini, kujituma na kutumia fursa zilizopo katika mazingira bora ya biashara yaliyowekwa na serikali.







Matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa miaka 15 ya Gs1 Tanzania. ambapo Kilele chaku kufanyika Septemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad