HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 14, 2026

Airtel Yazindua Kampeni ya Wese ni Bure Inayotoa Zawadi ya Mafuta Katika Vituo vya Mafuta Zaidi ya 62 Nchini

 



Dar es Salaam, Januari 2026.
KAMPUNI ya Airtel Tanzania leo imezindua kampeni ya Wese ni Bure ambayo inatokana na kampeni mama Inayoitwa Mwaka umenyooka na My airtel money app, Kampeni hii inalenga kuhamasisha matumizi ya miamala ya kidigital kupitia huduma ya Lipa namba kila unapoweka mafuta kwenye vituo vya mafuta zaidi ya 62 kote nchini ambavyo ni Mount Mero, ACER, Zebra Station na Bavuai.

Kampeni ya Wese ni Bure ni sehemu ya juhudi endelevu za Airtel Tanzania za kuwazawadia wateja wake, ikithibitisha dhamira ya kampuni ya kurahisisha malipo ya kila siku kwa njia salama na rahisi. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara wa Airtel Money, Bw. Emmanuel Moshi, alisisitiza umuhimu wa malipo ya kidijitali katika maisha ya kila siku akisema: “Kwa kuunganisha Airtel Lipa Namba kwenye malipo ya mafuta, tunaongeza thamani ya huduma za fedha kidijitali kwenye huduma moja muhimu sana ya kila siku, huku tukiwazawadia wateja wetu kwa kuchagua miamala salama na rahisi isiyotumia fedha taslimu.”

Akisisitiza dhamira hiyo kwa ngazi ya jamii, Meneja wa Malipo kwa Wafanyabiashara wa Airtel Money, Bw. Ismail Simanga, alieleza manufaa ya moja kwa moja ya kampeni ya Mwaka Umenyooka na My Airtel Money kwa wateja akisema: “Kampeni hii inaleta thamani halisi kwa wateja wetu kwa kubadilisha ununuzi wa kawaida wa mafuta kuwa fursa ya kupata zawadi, huku ikichochea matumizi ya malipo salama, ya haraka na rahisi ya kidijitali”

Kupitia kampeni hii, wateja watakaonunua mafuta katika vituo hivyo na kulipia kupitia Airtel Lipa Namba watapata nafasi ya kushinda lita 10 za mafuta bure kila wiki katika kipindi cha mwezi mmoja. Ili kushiriki, mteja anatakiwa kununua mafuta yenye thamani ya Shilingi 10,000 au zaidi na kulipa kupitia Airtel Lipa Namba, ambapo ataingizwa moja kwa moja kwenye droo ya kila wiki. Washindi watatangazwa kila wiki katika kipindi chote cha kampeni. Airtel Tanzania inaendelea kuonesha namna suluhisho za kifedha kupitia simu zinavyoweza kuongeza urahisi, ufanisi na ujumuishaji wa kifedha kwa kuziunganisha na mahitaji ya kila siku ya wateja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad