HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 5, 2025

Waziri Sangu Awataka MaDG Kuelekeza Mikakati Dira 20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo kuhakikisha kuwa mipango mikakati wanayoandaa na kuitekeleza inaendana moja kwa moja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.Amesema dhamira ya Serikali ni kuona taasisi zote zinachangia kikamilifu katika kujenga uchumi shindani wenye fursa pana na unaoendeshwa na rasilimali watu yenye ujuzi na tija.


Waziri Sangu amebainisha hayo Disemba 5, 2025 Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani kuitumikia Ofisi hiyo.

Amesisitiza kuwa Dira hiyo ni mwongozo muhimu unaoelekeza jinsi Tanzania itakavyofikia maendeleo endelevu katika kipindi kijacho.

Awali akizungumza Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Rahma Kisuo, amewasisitiza Wakurugenzi wa Taasisi hizo kuendelea kutoa elimu juu ya kazi zinazofanywa na Taasisi hizo.

Kwa Upande wao Wakurugenzi wa Taasisi hizo wamemhakikishia Waziri Sangu na Naibu Waziri Kisuo kuwa wako tayari kushirikiana nao kikamilifu katika kutekeleza majukumu ya Ofisi. 

Wameeleza kuwa maelekezo aliyoyatoa yatakuwa mwongozo muhimu katika kuboresha mikakati ya taasisi zao, huku wakiahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi na programu zinazolenga kujenga Taifa lenye rasilimali watu bora na uchumi imara.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad