HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 3, 2025

Rais Dkt. Samia Akutana na Kuzungumza na Naibu Mwenyekiti CWEIC Lord Hugo Swire Ikulu jijini Dar es Salaam

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara wa Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Lord Hugo Swire Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara wa Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025. Rais Dkt. Samia pamoja na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Lord Hugo Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza walijadiliana masuala ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira. Aidha, Lord Swire ameomba Tanzania kuwa mshirika wa kimkakati ili kuchochea wawekezaji wengi kutoka washirika wa Jumuiya hiyo ya Madola.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Mwenyekiti wa Biashara wa Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Lord Hugo Swire mara baada ya mazungumzo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad