Katika mazungumzo yao, Mhe. Dkt. Maghembe amempongeza Mhe. Sinimbo kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya kuiwakilisha nchi yake hapa Tanzania na kumhakikishia ushirikiano kutoka Wizarani na Serikalini kwa ujumla wakati wote atakapokuwa akitekeleza majukumu yake ya Ubalozi hapa nchini.
Kwa upande wake, Balozi Mteule, Mhe. Sinimbo amemshukuru Mhe. Maghembe kwa mapokezi mazuri na kueleza dhamira ya Serikali ya Namibia ya kuendelea kukuza ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa haya mawili.









No comments:
Post a Comment