IKIWA ni sehemu ya dhamira yake ya kuchangia maendeleo ya jamii, kampuni ya Meridiansport imeonesha moyo wa huruma kwa kukitembelea kituo cha watoto yatima cha Faraja Care Orphanage Centre kilichopo Mburahati na kugawa vifaa pamoja na mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaopatikana kituoni hapo.
Katika tukio hilo, Meridiansport ilitoa mahitaji muhimu ya shule kama mabegi, madaftari, vitabu na kalamu kama zawadi msimu wa sikukuu ili kuwawezesha watoto hao kufanya maandalizi mazuri kuelekea kuanza msimu mpya wa elimu hapo Januari.
Akiongea kwenye tukio hilo, Mwakilishi wa Meridiansport, Nancy Ingram alieleza kuwa kampuni hiyo haifanyi biashara tu, bali inajenga jamii.
Meridiansport inakupa taarifa mbalimbali za michezo ya kitaifa & kimataifa pamoja na uchambuzi wa michezo mbalimbali. Ingia leo kupitia meridiansport.co.tz na uanze kuburudika kwa taarifa mbalimbali za hapo kwa hapo ndani na nje ya nchi.
“Tunatambua kuwa watoto wetu wanakumbana na changamoto nyingi zinazorudisha nyuma maendeleo yao ya kimasomo. Kwa hiyo, tuliona ni muhimu kuchukua hatua ya kuwasaidia kwa vitendo. Tunataka kila mtoto ajisikie salama na mwenye kupewa upendo na kuthaminiwa.”
Wanufaika wa msaada huo walipokea vifaa kwa furaha na shukrani, wakieleza kuwa msaada huo utawapa ujasiri wa kuendelea na masomo yao bila hofu wala vikwazo vya kimahitaji ambavyo kwa namna kubwa vimekua vikiwarudisha nyuma.
Hatua hii ni sehemu ya mfululizo wa miradi ya kijamii inayotekelezwa na Meridiansport, ikilenga sekta mbalimbali kama afya, elimu na mazingira. Meridiansport inaendelea kuthibitisha kuwa uwajibikaji kwa jamii ni sehemu ya utendaji wake.



No comments:
Post a Comment