Katika safari hizo mpya, shirika hilo limetangaza ofa ya tiketi ya kurudi (return ticket) kwa USD 499, ambapo abiria wa Daraja la Biashara (Business Class) wanaruhusiwa kubeba mizigo yenye uzito wa hadi kilo 69, huku Daraja la Kawaida (Economy Class) likiruhusu mizigo ya hadi kilo 46.
Kuanzishwa kwa safari za Victoria Falls kunaifanya Air Tanzania kupanua mtandao wake wa safari nchini Zimbabwe, ambapo mji huo unakuwa kituo cha pili (second destination) baada ya Harare, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo wa kuongeza safari za kimataifa na kukuza utalii, biashara na usafiri wa kikanda.
Hatua hiyo pia inatarajiwa kuchochea zaidi sekta ya utalii, hasa kwa kuunganisha vivutio vikubwa vya utalii vya Afrika Mashariki na Kusini, ikiwemo Maporomoko ya Victoria Falls, moja ya maajabu ya dunia.









No comments:
Post a Comment