HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 26, 2025

WAZIRI KAPINGA: TUTAENDELEA KUWEZESHA BIASHARA NDOGO NA VIWANDA VYA KATI

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), ameliagiza Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) kuongeza ubunifu na kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utekelezaji wa majukumu yake, ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na kuongeza tija katika sekta ya viwanda.

Waziri Kapinga alitoa maagizo hayo Novemba 26, 2025, alipotembelea makao makuu ya SIDO jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Bodi pamoja na Menejimenti ya shirika hilo. 

Amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kuwezesha viwanda vidogo na biashara ndogo kukua, kuimarika na kuongeza ajira kwa vijana.

Amesisitiza kwamba mifumo ya kidijitali itaiwezesha SIDO kuwa na takwimu sahihi za viwanda vidogo nchini, hatua itakayosaidia Serikali kupanga mikakati ya maendeleo kwa usahihi na ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, amesema SIDO ni uti wa mgongo wa maendeleo ya viwanda vidogo na mshirika muhimu wa Serikali katika kutekeleza ajenda ya uchumi wa viwanda.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya SIDO, Prof. Mussa Nyamsingwa, ameihakikishia Serikali kuwa Bodi na Menejimenti ya shirika hilo wako tayari kutekeleza maelekezo yote kwa ufanisi, ili kuhakikisha sekta ya viwanda vidogo na biashara ndogo inaendelea kukua na kuchangia ajira kwa vijana nchini.














No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad