Wajumbe wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Tuzo za Uhifadhi na Utalii 2025 wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Utalii Richie Wandwi wameendelea na zoezi la uhamasishaji na utoaji elimu kwa wadau wa utalii na uhifadhi juu ya tuzo za Serengeti zinazotarajiwa kufanyika mwezi Desemba 2025.
Zoezi hilo linalolenga kuwajengea uelewa wadau juu mambo muhimu ikiwemo, kategoria za tuzo na namna ya kujisajili na kuwa mshiriki wa tuzo hizo limefanyika Jumatatu Novemba 17 Jijini Arusha kwa Kanda ya Kaskazini.












No comments:
Post a Comment