HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 27, 2025

Prof. Palangyo: Kila mtu ana wazo la kipekee, likiweka kwenye maandiko

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, Prof. Eunice Palangyo, amewataka vijana kutumia akili zao asilia katika kuandika kazi bunifu na maandiko ya kisanaa, ikiwemo makala za jarida, badala ya kutegemea akili bandia (Artificial Intelligence – AI).

Wito huo umetolewa leo Novemba 27, 2025 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Waandishi yanayofanyika kila Novemba chuoni hapo.

Prof. Palangyo amesema kuwa lengo kuu la siku hiyo ni kutoa hamasa kwa vijana, watoto na watu wazima kuunda maandiko bunifu sambamba na kuinua hali ya usomaji wa vitabu katika jamii.

“Kila mtu ana wazo, kila mtu ana kitu cha kuandikwa; kile kinaposomwa na wengine kinazaa mambo mengine mengi. Tunataka hali ya kupenda kusoma iwe asili yetu,” alisema Prof. Palangyo.

Ameongeza kuwa matumizi ya akili ya asili yana nafasi kubwa na ya kipekee isiyofananishwa na kitu kingine, hususani katika uandishi bunifu.

Kwa upande wake, Prof. Fredrick Mtenzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, amesema kuwa AI itumike kama chombo cha msaada katika uandishi, si kuchukua nafasi ya mawazo ya kibunifu ya mwandishi.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad