Sehemu ya wafanyakazi wa TTCL wa Tawi la Kijitonyama wakijumuika. |
Baadhi ya wateja wa TTCL wakizungumza kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025, yaliofanyika Ofisi za taasisi hiyo Tawi la Kijitonyama jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya wateja wa TTCL wakizungumza kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025, yaliofanyika Ofisi za taasisi hiyo Tawi la Kijitonyama jijini Dar es Salaam. |
Meneja wa TTCL Kijitonyama, Bw. Diwani Mwamengo akizungumza kwenye hafla hiyo |
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania - TTCL, limefunga Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 kwa kusherekea pamoja na wateja wake waliofika siku ya leo kupata huduma katika Ofisi za taasisi hiyo Tawi la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo wateja walishiriki kukata keki maalum pamoja na kunywa shampeni iliyoandaliwa kwa wateja tawini hapo.
Akizungumza katika hafla hiyo, ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025, Meneja wa Biashara Shirika la TTCL, Bw. Humphrey Ngowi alisema wiki ya huduma kwa wateja imetoa fursa ya TTCL kutathmini mafanikio yao na kuainisha maeneo ya kuboresha na kujifunza njia bora zaidi ya kutimiza mahitaji ya wateja wao.
"...Pia imekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu na kuimarisha ari ya timu miongoni mwa wafanyakazi wetu kuanzia viongozi wakuu hadi wale wa ngazi za chini. Kwa miaka mingi TTCL imeendelea kuwa nguzo ya mawasiliano nchini Tanzania, ikitoa huduma muhimu zinazounganisha Watanzania mijini na vijijini, Hata hivyo katika dunia ya sasa inayobadilika kwa kasi tunatambua haja ya kuendelea kuboresha mifumo yetu, kutumia teknolojia za kisasa, na kuongeza thamani katika huduma tunazozitoa kila siku," alisema Bw. Ngowi.
Alisema kwa mwaka huu 2025, TTCL imeendelea kufanya maboresho makubwa katika mafumo yetu ya mawasiliano kupitia miradi ya kimkakati ikiwa ni pamoja na kupanua huduma vijijini na mijini na kuendeleza upanuzi wa mkongo wa taifa wa mawasiliano na kusimamia ujenzi wa minara mipya.
Aidha alibainisha kuwa, wiki ya huduma kwa wateja imeacha alama katika shirika letu kwani imekuwa fursa ya kupata mrejesho kutoka kwa wateja kutambua mapungufu, na kuandaa maboresho yanayolenga kikidhi maitaji halisi ya wateja wetu. Napenda kutoa shukrania kwa kila mmoja aliyefanikisha kukamilika kwa maadhimisho haya. "Wateja wetu ndio wamechangia kiasi kikubwa ya sisi kuwa hapa na kupitia kwao tunathibitisha kuwa; “Mission: Possible” si kauli mbiu tu bali ni uhalisia tunaoishi kila siku.
Aliongeza kuwa TTCL itaendelea kutoa huduma bora za kuaminika zenye ubora wa hali ya juu, tutaendelea kusikiliza maoni ya ya wateja wetukuboresha huduma zetu, na kuhakikisha kila mmoja wetu anapata thamani stahiki ya huduma anazostahili.
No comments:
Post a Comment