HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 7, 2025

Teknolojia ya Vizimba Yaokoa Mamia Kanda ya Ziwa

Na Mwandishi Wetu, Busega

Kama wanavyosema Taasisi ya Mckensey katika andiko lao mashuhuri duniani lenye anuani ya “Voices On Society: The Art and Science Of Delivery,” kuwa katika mipango yote lazima mwishowe kulinda utu na maendeleo ya watu, Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza hilo Kanda ya Ziwa.

Leo Oktoba 7, 2025, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amefika wilayani Busega, Simiyu kujionea jinsi mikakati ya Serikali kuwakinga wananchi dhidi ya hatari za mamba na viboko Ziwa Victoria inavyoakisi uhalisia.

“Hapo ikiwa ni mushabaha wa maeneo mengine nchini nimejionea kina baba, kina mama na watoto wakitumia vizimba hivi kwa amani kabisa wakifua, kuchota maji, kuogelea na sasa naambiwa mandhari za ndani za vizimba hivi yameanza kutumika kama maeneo ya kubarizi,” anasema Dkt. Abbasi.

Teknolojia hii ya vizimba vya chuma imebuniwa na wataalam wa Wizara na inaendelea maeneo mbalimbali yenye hatari hizi nchini iwe kwenye mito au maziwa na ukanda huu tu wa Ziwa Victoria tayari kuna vizimba zaidi ya 15 vilivyokamilika, vingi zaidi vinaendelea kujengwa na mwaka huu imeshatengwa bajeti ya vizimba zaidi ya 50 maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali inapitia upya Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Wanyama Wakali na Waharibifu wakiwemo tembo, fisi, simba, chui, mamba na viboko.

Tanzania imetenga takribani theluthi moja ya eneo lake la ardhi kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori; chanzo kikuu cha utalii nchini.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad