HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 12, 2025

TBS YATEKETEZA TANI 1.53 YA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati, Dodoma, limeteketeza jumla ya tani 1.53 za bidhaa za chakula ambazo hazijakidhi matakwa ya viwango, zikiwemo zilizokwisha muda wa matumizi.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika Oktoba 11, 2025, Afisa Udhibiti Ubora wa TBS Kanda ya Kati, Daniel Marwa, alisema bidhaa hizo zenye thamani ya shilingi milioni 8.11 zilikamatwa katika ukaguzi mbalimbali uliofanyika kati ya Julai hadi Oktoba 2025 katika mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa.

Marwa alisema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za TBS kulinda afya za watumiaji na kuhakikisha bidhaa zote zinazouzwa sokoni zinakidhi viwango vilivyowekwa kisheria.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad