HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 17, 2025

RC KUNENGE: TUNATAKA PWANI YA KUTATUAMIGOGORO KWA UBUNIFU WA KIMKAKATI

 




Na Khadija Kalili , Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge, amesema serikali ya Mkoa imelenga kuifanya Pwani kuwa kinara wa ubunifu na utatuzi wa changamoto kwa njia za kimkakati, ili kuongeza tija katika utoaji huduma na kuvutia uwekezaji.

Mhe. Kunenge ametoa kauli hiyo leo tarehe 17 Oktoba alipokua mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo ya kujengea uwezo viongozi wakuu wa sehemu na vitengo wa Halmashauri ya Chalinze, yaliyofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha.

Amesema viongozi wanapaswa kutumia maarifa waliyojifunza ili kuleta matokeo chanya katika maeneo yao ya kazi, kwa kuibua fursa mpya na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji.

“Tujitahidi kutumia mafunzo haya kutengeneza fursa na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji.

Tunataka kuona matokeo chanya ya mlichojifunza hapa,” amesema Mhe. Kunenge.

“Mkoa wa Pwani unataka kuwa eneo la ubunifu na suluhisho endelevu kwa changamoto zinazoukabili.”amesema RC Kunenge.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Pili Mnyema, amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kuendeleza mawazo ya kimkakati yatakayowezesha utekelezaji wa miradi bunifu ya maendeleo, ili kupunguza utegemezi kwa Serikali Kuu.

Amesisitiza umuhimu wa viongozi kuendana na mabadiliko ya teknolojia na kutumia mbinu mpya za usimamizi ili kuongeza ufanisi na tija katika utoaji wa huduma.

Mafunzo hayo ya siku tano yamejikita katika kuimarisha uwezo wa viongozi kwenye masuala ya uongozi, ubunifu, utatuzi wa changamoto, na usimamizi wa rasilimali, yakiwa na lengo la kuboresha utoaji huduma kwa wananchi na kuchochea maendeleo endelevu katika Halmashauri ya Chalinze na Mkoa wa Pwani kwa ujumla.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi amesema kuwa wamepokea maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliyewataka kuwa wabunifu katika kuvutia wawekezaji ndani ya Halmashauri hiyo.

"Chalinze tumejipanfa hadi sasa tunayomaeneo ya viwanda zaidi ya 300 na yote yameshapimwa hii yote ikiwa ni katika kuchangamkia fursa kwa wawekezaji ndani ya Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani pia tunaona fursa nyingi zinakuja kwetu.

" Kama mlivyoona hivi karibuni Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuja kuzindua bandari kavu ya Kwala ambayo ni sehemu yetu ya uwekezaji hivyo tumeanza kuboresha eneo la Vigwaza kwa kuweka miundombinu rafiki kwa wawekezaji ambayo itawavutia pia mwekezaji akija atasema huduma anayohitaji ibireshwe na sisi tutatimiza" amesema Possi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad