
Na Khadija Kalili, Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025.
RC Kunenge amesema hayo leo asubuhi aalipoongea katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo Mkoani hapa.
" Pwani tumejipanga kudhibiti kikundi ama mtu yeyote ambaye atakua na nia ovu ya kuleta vurugu siku ya uchaguzi, wananchi jitokezeni bila ya kuwa na hofu nendeni mkapige kura kisha rudi nyumbani" amesema .
Natumia nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na mamlaka aliyokuwa nayo ametangaza siku ya kupiga kura kuwa siku ya mapumziko jambo ambalo litaleta utulivu wa watu kwenda kupiga kura.
" Tarehe 29 Oktoba 2025 itakua siku rasmi kwa watanzania kwenda kupiga kura kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani katika mjimbo husika, Serikali tumefanya maandalizi ya kutosha kwa kushirikiana na Viongozi wa dini na mazingira mazuri ya kwenda kupiga kura ambapo kwa Mkoa wa Pwani ina vituo vya kupigia kura 3941 ambavyo vyote vipo jirani na maeneo wanayoishi wananchi.
" Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejipanga vizuri , natoa onyo kwamba tunazo taarifa za kila eneo ndani ya Mkoa wa Pwani na tunaju nini kitaendelea wananchi nendeni mkatekeleze haki yenu kikatiba" amesema RC Kunenge.
Wakati huohuo ametoa shukrani kwa Waandishi wa Habari ambao wamekua wakifanya kazi kubwa ya kuelelimisha jamii.
Wakaazi wote wa Mkoa wa Pwani shime jitokezeni kushiriki uchaguzi na siku ya uchaguzi ni moja tu amkeni mapema muwahi kwenye vituo vya kupiga kura ambavyo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi jioni utakapofika mwisho wa kupiga kura kila atakayekuwa katika foleni atapiga kura" amema Kunenge.

No comments:
Post a Comment