HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 29, 2025

Meridianbet Yaendeleza Mapambano Dhidi Ya Saratani Ya Matiti

 


KILA mwezi wa Oktoba, rangi ya waridi huvaa sura mpya duniani kote, ni mwezi wa kuhamasisha mapambano dhidi ya saratani ya matiti. Kwa Meridianbet, huu si tu mwezi wa kampeni, ni muendelezo wa dhamira ya kweli ya kusaidia jamii.

Kupitia mpango wake wa kila mwaka wa “Tuko Pamoja Nanyi”, Meridianbet imeendelea kutoa msaada wa vitendo kwa wanawake kupitia huduma za bure za uchunguzi wa saratani ya matiti. Safari ya mwanamke mmoja nchini Montenegro, aliyepata huduma bila usumbufu wowote, bila fomu, wala ada. Hii inabeba kiini cha falsafa ya kampuni, kufika moja kwa moja kwa wahitaji.

Kampeni hii ni sehemu ya mfumo mpana wa uwajibikaji wa kijamii wa Meridianbet, unaotekelezwa katika masoko 18 duniani, chini ya kampuni mama Golden Matrix (NASDAQ: GMGI). Kupitia jukwaa la ubunifu Meridian Donate, wateja wanaweza kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali kwa urahisi kupitia QR code au kifaa cha michango kilichojumuishwa kwenye michezo. Hapo ndipo teknolojia inakutana na utu.

Meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Meridian Donate limeleta mageuzi makubwa, michango sasa inajumuishwa moja kwa moja katika uzoefu wa michezo ya kubahatisha. Wateja wakicheza, wanachangia fedha zinakwenda moja kwa moja kwenye hospitali za uzazi, usafi wa mazingira, na miradi ya vijana.

Takwimu zinaonyesha matokeo halisi, mwaka 2024 pekee, kampuni ilitekeleza vitendo 293 vya kijamii, ikilinganishwa na 257 mwaka 2022. Mashirika 212 yalipokea msaada kupitia kampeni 43 likiwa ni ongezeko maradufu kutoka mwaka uliopita.

Kwa Meridianbet, uwajibikaji wa kijamii si nadharia. Wafanyakazi wanashiriki moja kwa moja kutoa msaada wao binafsi. Mwaka 2024, walijitolea zaidi ya saa 5,000 katika miradi ya kijamii, huku kampuni ikiendelea kuongeza ajira kwa watu wenye ulemavu (hadi 39 kwa sasa).

Tangu kuanzishwa kwa Msingi wa Meridianbet (Meridian Foundation) mwaka 2020, zaidi ya vituo 40 vya afya vimepata msaada. Hivi karibuni, mpango wa utoaji vitabu ulizinduliwa baada ya mfanyakazi mmoja kuguswa na changamoto za maktaba maskini, ndani ya wiki chache, maelfu ya vitabu vilikusanywa na kusambazwa katika masoko yote 18.

Mfumo wa Meridian Donate unathibitisha kuwa mabadiliko makubwa hayatokani na misaada mikubwa, bali miundombinu midogo inayofanya kazi kwa ufanisi. Kwa Meridianbet, kila dau ni fursa ya kutoa tumaini. Tuko pamoja nanyi. Daima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad