Na Khadija Kalili
MJUMBE Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Alhaji DKT. Chakou Khalfan Tindwa leo tarehe 26 Oktoba 2025 amewaomba wananchi wa Kata ya Makurunge iliyopo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani kujitokeza kwa wingi kupiga kura 29 Oktoba 2025.
Dkt. Tindwa amemuombea kura za ndiyo kutoka kwa wananchi waliojitojeza leo kwenye ufungaji wa kampeni huku akimnadi mgombea wa kiti cha Ubunge wa jimbo hilo Dkt. Selemani Jafo ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Diwani Wakili Msomi Aidan Kitake wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi za Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la Kisarawe Mkoani Pwani.
" Ndugu wananchi wa Makurunge nawasihi ifikapo (Jumatano ijayo) tarehe 28 Oktoba 2025 usitoke pekeako toka na familia ili wote mkachangue mafiga matatu ya Chama Cha Mapinduzi ambayo (CCM),ambayo ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wetu Dkt. Selemani Jafo na Diwani Wakili Msomi Aidan Kitale" amesema Dkt. Tindwa.
" Nimesimama hapa nikiwa mdau mkubwa wa Makurunge kwani nina miliki maeneo matatu ikiwa ni pamoja na eneo ambalo nitajenga sheli ( Petroli Station) na haipiti miezi mitatu sijaja Makurunge" amesema Dkt. Tindwa.
" Makurunge ni kati ya maeneo kumi bora ambayo yamefikiwa na umeme ndani ya jimbo hili , mwezi uliopita nilikua nchini Zambia vijijini kwenye shughuli zangu sina budi kusema nchi yetu iko mbali katika masuala miundombinu kama umeme, barabara na afya ukilinganisha na nchi za jirani na hii yote inatokana kuwa na Uongozi madhubuti wa CCM hivyo ji jambo la kujivunia" amesema Dkt. Tindwa.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa Kamati ya Mikakati Umoja wa Wanawake Tanzania
(UWT) Kanda ya Mashariki inayoùndwa ja Mikoa ya Dar es Salaam , Tanga, Morogoro na Pwani Mhe. Sofia Simba amesema kuwa katika historia miaka yote Mkoa wa Pwani umekua ukishika nafasi ya tano kwenye matokeo ya uchaguzi mkuu, kwa mwaka huu ikibidi Mkoa ukashike namba moja na anaimani kwamba itawezekana.
"Namuombea kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kiti cha Rais , pia namuombea kura mwanangu wa kumzaa mwenyewe Dkt. Selemani Jafo anayewania kiti cha Ubunge na Wakili Msomi Aidan Kitale" amesema Mhe.Simba.
" Ifikapo tarehe 29 Oktoba Mwaka huu (Mtondo) kahakikisheni mnakwenda kupiga kura na usitoke pekeako toka na familia yako na mkaichague CCM kwa sababu ni Chama chenye uzoefu wa kuongoza.
Naye Katibu Kamati ya Mikakati UWT Kanda ya Mashariki Mhe.Hawa Abdulrahman Ghasia amewaeleza wananchi wa Makuringe kamwe wasitishike na kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kwamba siku hiyo kutakua na fujo.
" Kamwe msitishike na Kauli za mitandaoni hakuna kitu kibaya kitakachotokea kwani miongoni mwa wagombea wenye uzoefu kuliko wote ni mgombea wa kiti cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa CCM, yeye anajua kila anachokiomba kwa wananchi tofauti na wagombea wengine ambao uzoefu wao ni kutoa lugha za kebehi, matusi, maandamano na kulala gerezani tena huku familia zao zikiwa ziko nje ya nchi" amesema Ghasia.
Mgombea kiti cha Ubunge Dkt. Jafo amewasisitiza wananchi wa Makurunge Jimboni Kisarawe kujitokez kwa wingi kwenye siku ya uchaguzi na kusisitiza wamchague Mhe.Rais Dkt. Samia yeye Mbunge wa Kisarawe na Diwani wa Kiluvya Kitale.
Kitale amesema kuwa anatoa shukrani kwa timu ya kampeni Wilaya ya Kisarawe Moani Pwani huku akiomba kura za mafiga matatu ambazo ni nafasi ya Rais, Mbunge na Diwani.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
No comments:
Post a Comment