Rai hiyo imetolewa Septemba 23, 2025 na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhandisi Enock Nyanda wakati wa kufungua kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Uhimili na Kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi (LoCAL).
Amesema upo umuhimu kwa taasisi za umma nchini kuhakikisha zinandaa program na mipango kazi yenye vipaumbele vinavyoakisi ajenda mahsusi ya mazingira na mabadiliko ya tabia katika maeneo yao ya kazi.
Mhandisi Nyanda amesema ili kufanikisha ajenda hiyo iliyoanishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo, Serikali itahakikisha wadau wote wanajumuishwa ili kuandaa mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili kufanikisha utekelezaji wake.
“Dira imezinduliwa na wajibu wetu kuhakikisha tunaandaa vipaumbele vya mipango ya maendeleo yenye ajenda ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi ili kupima matokeo ya utekelezajii wake kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050” amesema Nyanda
Kuhusu Mradi wa LoCAL, Mhandisi Nyanda amesema mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2017 umeleta mafanikio makubwa katika afua za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika ngazi za msingi.
Amesema Shirika la Umoja wa mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) lilianza mradi huo kwa majaribio ya awali ili kupima mbinu ya kuelekeza fedha za mabadiliko ya tabianchi kwa halmashauri chache kabla ya kupanua uwigo na kufikia halmashauri nyingi zaidi
Ameeleza kufuatia mafanikio yaliyopatikana, katika awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi UNCDF imepanga kupanua wigo wa utekelezaji kutoka Halmashuri tatu hadi kufikia halmashauri nane nchini.
Amezitaja Halmashauri za Wilaya zitakazonufaika na awamu ya pili ya Mradi wa UNCDF-LoCAL kywa ni Mkinga (Tanga), Mtama (Lindi), Kigamboni (Dar es Salaam), Mafia (Pwani) na Mtwara (Mtwara).
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa UNCDF-Local nchini Tanzania, Bi. Aine Mushi amesema Shirika la UNCDF inaoendelea kuupata kutoka kwa Serikali hatua inayowezesha Mradi huo kuendelea kuleta manufaa kwa jamii.
“Mradi huu hautazitangaza Halmashauri pekee, bali pia utajenga ushawishi kwa Mashirika ya kimataifa kufahamu dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi” amesema Bi. Mushi.
Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sanford Kway amelishukuru Shirika la UNCDF kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Serikali ya Tanzania inatekeleza Mpango wa UNCDF wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (LoCAL), ambao unatumia Ruzuku za Ustahimilivu wa Tabianchi zilizopangwa kwa Utendaji (PBCRGs) kuelekeza fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kutumia mifumo ya uhamasishaji ya kitaifa.
Mmoja wa wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri elekezi Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL, Bi. Magdalena Sikwale kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akichangia mada wakati wa kikao hicho kilichofanyika Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.
Mmoja wa wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri elekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL, Bw. Stephano Umbilo kutokaWizara ya Kilimo akichangia mada wakati wa kikao cha washauri walekezi wa mradi huo kilichofanyika Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.Mmoja wa wajumbe wa kikao kazi cha mapitio ya utekelezaji wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL, kutoka Shirika la UNCDF, Bi. Catherine Russel akichangia mada wakati wa kikao kazi wadau na washauri walekezi wa mradi huo kilichofanyika Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhandisi Enock Nyanda akizungumza na wajumbe wa kikao kazi cha kikao kazi cha wadau na washauri washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL kilichofanyika Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha cha wadau na washauri elekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakifuatilia majadiliano mbalimbali wakati wa kikao kazi cha mradi huo kilichofanyika Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.
Mratibu wa Mradi wa UNCDF-Local nchini Tanzania, Bi. Aine Mushi akizungumza na wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL kilichofanyika Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya ufunguzi wa kikao hicho Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha wadau na washauri elekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL wakifuatilia majadiliano mbalimbali wakati wa kikao kazi cha mradi huo kilichofanyika Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.Afisa Misitu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sanford Kway akizungumza wakati wa kikao kazi cha wadau na washauri walekezi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL kilichofanyika Septemba 23, 2025 Jijini Dodoma.
(Na Mpigapicha Wetu)
(Na Mpigapicha Wetu)
No comments:
Post a Comment