Pwani, Septemba 24, 2025 – Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mariam Ibrahim, ameungana na Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Pwani katika maandalizi ya kumkaribisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mariam ametembelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo akihamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kumpokea Rais Samia, huku akitoa pongezi kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa chini ya uongozi wake.
“Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia kwa mambo makubwa aliyoyafanya Mkoa wa Pwani. Kupitia uongozi wake tumepata fedha za kukamilisha miradi ya maji, shule za sekondari na msingi, hospitali, vituo vya afya, zahanati, pamoja na kupeleka umeme katika kila kijiji. Pia tumeshuhudia upanuzi wa barabara kutoka Mbagala Rangitatu hadi Mkuranga baada ya kupata kibali kutoka kwake,” alisema Mariam.
No comments:
Post a Comment