Katika ziara hiyo, wageni walipata nafasi ya kuona vivutio mbalimbali vikiwemo maporomoko ya maji, mimea ya kipekee na mandhari ya Mlima Kilimanjaro maarufu kama “Paa la Afrika”.
Katibu wa TUGHE, Hery Mkunda, alisema kuwa ziara hiyo imewapa uelewa mkubwa zaidi wa thamani na uzuri wa urithi wa dunia.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Steria Ndaga, aliwapongeza TUGHE kwa kuunga mkono utalii wa ndani, akibainisha kuwa kutembelea hifadhi kunasaidia kuongeza pato la taifa na ajira kwa vijana.
Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TANAPA, Jully Bede Lyimo, aliongeza kuwa utalii wa ndani una faida nyingi zikiwemo kuongeza mapato, kuchochea ajira, kukuza biashara ndogo ndogo na kujenga uzalendo wa taifa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Amri Mtekanga, aliwakaribisha wageni hao na kuwaeleza vivutio pamoja na taratibu za kupanda Mlima Kilimanjaro.
Ziara hiyo ya TUGHE imedhihirisha mshikamano wa Watanzania katika kuunga mkono sekta ya utalii kuelekea maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani.










No comments:
Post a Comment