Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025 kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya usalama yenye haki.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita,James Ruge amesema hayo wakati wa semina ya maafisa uchaguzi ngazi ya jimbo na wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata kwa majimbo ya Geita na Geita Mji ambapo wanapaswa kusimamia kwa umakini na uadilifu malalamiko yote ya uchaguzi kwa uwazi.
“Ni jukumu lenu kuhakikisha hakuna vitisho, hakuna ununuzi wa kura na hakuna upendeleo siku ya kupiga kura. Baada ya kura kupigwa, msimamie kwa uwazi na mshughulikie malalamiko kwa haki,” amesema Ruge.Kwa upande wake, Afisa kutoka Takukuru,Said Lipunjaje wakati akiwasilisha mada ya sheria za uchaguzi amewataka wasimamizi kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ili kuepuka kusababisha matokeo kubatilishwa.
Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Geita, Sarah Yohana, amesema maadili ya uchaguzi yanatakiwa kusimamiwa kwa uwazi bila upendeleo wa chama wala mgombea yeyote.
No comments:
Post a Comment