Elimu hiyo imetolewa kwa wananchi kuanzia 8-9 Septemba, 2025 kwa vijiji hivyo huku ikifuatiwa na ukaguzi utakaofanyika katika mgodi huo ikiwa ni hatua ya awali ya kuelimisha jamii na wawekezaji kabla ya Mradi huo kuanza ambapo ni maagizo yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha jamii inatambua uwepo wa Mradi huo na kuhakikisha jamii haiathiriki na Mradi huo.
Akizungumza katika utoaji wa elimu hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi, Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria (NEMC) Bw. Jamal Baruti ameutaka Uongozi wa vijiji kutumia Kamati za Mazingira na kushirikiana na Serikali kuendelea kuelimisha jamii juu ya maswala ya Mazingira na Afya ya jamii yanayoweza kusababishwa na Mradi huo.
Kwa upande wake, Meneja Kanda ya Kusini (NEMC) Bw. Boniface Guni amewataka wakazi wa vijiji hivyo kuchangamkia fursa za ajira katika Mradi huo huku wakizingatia ulinzi wa Afya zao na Mazingira.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria NEMC Bw. Jamal Baruti amesema NEMC itaendelea na ufuatiliaji wa maswala ya kimazingira kwa kushirikiana na Taasisi nyingine huku akiitaka Kampuni ya Mantra TZ LTD ya Uchimbaji katika mgodi huo kutambua haki za wakazi wa vijiji hivyo na kuchangia shughuli za maendeleo ya wakazi wa vijiji hivyo kama manufaa ya Mradi huo.










No comments:
Post a Comment