Mshindi wa Mnada wa PIKU, Jenipher Ayoub katikati akiwa na zawadi zake mara baada ya kukabidhiwa leo Septemba 06, 2025 Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya zawadi na washindi wa kizipokea zawadi zao.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa PIKU Afrika, Barnabas Mbunda katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 06, 2025 mara baada ya kuwatangaza washindi wa zawadi za Mnada wa PIKU.JUKWAA la Kidijitali la PIKU Afrika, linaloendesha minada ya kipekee mtandaoni, leo Septemba 6, 2025 limetangaza na kukabidhi zawadi kwa washindi wa awamu ya pili ya promosheni yake.
Mshindi wa kwanza, Jenipher Ayoub, amejinyakulia zawadi kubwa zikiwemo friji, jiko janja lenye sahani nne (tatu za gesi na moja ya umeme), mashine ya kufulia, vifaa vya jikoni pamoja na kifaa cha kuchakata vyakula (food processor).
Mshindi wa pili, Michel Ezekiel, amepokea simu, bando la mwaka mzima kutoka Airtel na spika za bluetooth, huku mshindi wa tatu, Niyovita Shayo, akijishindia seti ya vipodozi na saa ya kike ya mkononi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa PIKU Afrika, Barnabas Mbunda, amesemaa awamu ijayo ya mnada itakuwa ya kipekee zaidi kupitia mpango wa Zigo la Piku.
“Baada ya siku 28, mshindi atakayetoa dau dogo na la kipekee atajipatia pikipiki mpya aina ya TVS yenye helmeti, reflector, kadi ya mafuta ya miezi sita na bima, pamoja na gari aina ya Raum,” amesema Mbunda.
Mbunda ameongeza kuwa lengo la PIKU ni kupanua wigo wa huduma na kuhakikisha kila mshiriki anapata nafasi ya kushindania bidhaa zenye thamani kubwa.
Aidha, ameeleza utaratibu wa ununuzi wa tiketi ambapo tiketi 10 zinapatikana kwa Sh.1,000, tiketi 50 kwa Sh.5,000, tiketi 100 kwa Sh.10,000 na tiketi 1,000 kwa Sh.100,000, akibainisha kuwa kadri tiketi zinavyoongezeka ndivyo nafasi ya ushindi inavyokuwa kubwa zaidi.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Vivian Mboya, amesema mnada huo umefanyika kwa kufuata kanuni na taratibu rasmi, na washindi wote wamepokea zawadi zao kihalali.
“Ni kweli washindi wamepata zawadi zao kwa kufuata taratibu, sheria na vigezo vilivyowekwa kama ilivyotangazwa awali,” amesema.
Akieleza furaha yake, mshindi wa kwanza Jenipher Ayoub, ambaye alitoa dau la Sh.36,000 pekee na kushinda bidhaa zenye thamani ya Sh. milioni 4 kutoka kampuni ya LG, ameipongeza PIKU Afrika kwa kuendesha minada ya kweli mtandaoni.
“Niliona tangazo Instagram, nikaamua kujaribu, na hatimaye nikashinda zawadi ambazo sikutegemea. Nawashukuru sana PIKU,” amesema kwa furaha.
No comments:
Post a Comment