Ikiwa ni jitihada za kufungua fursa za kimaendeleo kwa Watanzania, Kampuni ya Piga Beti inaendelea na kampeni maalum ya promotion inayowapa washiriki mbalimbali nafasi ya kujishindia zawadi kubwa ikiwemo magari na simu janja (smartphones) kila wiki.
Afisa Msaidizi wa Wateja wa Piga Beti, Hemed Misonge, ameeleza kuwa kampeni hiyo imekuwa chachu ya kufungua milango ya fursa hususan kwa vijana, ambapo kila Alhamisi washindi huibuka na zawadi za thamani kupitia promosheni zinazofanyika nchi nzima.
Miongoni mwa washindi waliopokea zawadi hivi karibuni ni:
Anthony Mkondoa, aliyejinyakulia Smartphone Samsung Galaxy A16 kupitia kampeni ya Jismartishe na Mix by Yas.
Godwin Mbarouk, mshindi wa Samsung Galaxy A26 5G, pia kupitia kampeni hiyo.
Issa Haruna, aliyeibuka na Smart TV Hisense 55 Inches kupitia kampeni ya Shinda Ndinga.
Hemed Misonge alisisitiza kuwa kampeni hizo ni endelevu na zinatarajiwa kufikia tamati mwezi Novemba, huku wateja wa Piga Beti kote nchini wakiendelea kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila wiki.
No comments:
Post a Comment