Dar es Salaam, Septemba 26, 2025 – Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeshiriki katika Maonesho ya 22 ya Wahandisi yanayoendelea katika viwanja vya Mlimani City, ambapo wanafunzi wake wametumia fursa hiyo kuonesha ubunifu wao kwa wananchi.
Akizungumza katika maonesho hayo, mwanafunzi wa shahada ya Uhandisi wa Umeme, Mohamed Chipokoso, amesema maonesho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kuonesha bunifu zinazoweza kusaidia jamii.
Chipokoso ameonesha mfumo maalum wa teknolojia unaoweza kudhibiti vifaa vya umeme majumbani, kama vile taa na feni, kwa kutumia simu ya mkononi.
Mfumo huo unamwezesha mtumiaji kuwasha au kuzima vifaa vya umeme hata akiwa mbali na nyumbani, hatua itakayosaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya umeme na kuongeza usalama wa nyumba.
“Mfumo huu ni rahisi kutumia kwa kuwa unaweza kufanya kazi kwa kutumia simu yoyote. Mfano, mtu akitoka nyumbani na kusahau kuzima taa au feni, anaweza kutuma ujumbe mfupi na mfumo utaweza kuzima vifaa hivyo mara moja,” amesema Chipokoso.
Amefafanua kuwa teknolojia hiyo inaweza kufanya kazi hata ukiwa mkoa mwingine au nje ya makazi, mradi tu mfumo uwe umefungwa nyumbani.
Hata hivyo, Chipokoso amebainisha changamoto zinazowakabili wabunifu wengi nchini, ikiwemo ukosefu wa mtaji na wadau wa kuwaunga mkono ili kufanikisha mawazo yao.
“Wapo vijana wanaoibua mawazo makubwa lakini hukosa msaada wa kifedha na kiufundi kuyapeleka sokoni. Hii ndiyo sababu bunifu nyingi hubaki kwenye karatasi au maabara za vyuo,” amesema.
Aidha, amewahimiza vijana wenzake kuendelea kubuni bila kukata tamaa, akisisitiza kuwa si kila wazo linahitaji gharama kubwa, na kwamba kujaribu mara kwa mara ni njia ya kufanikisha ndoto.

No comments:
Post a Comment