HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 5, 2025

JALI USALAMA WAKO NA WA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA - RTO PWANI

 


MKUU wa kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Edson Mwakihaba amewataka maafisa usafirishaji wa Mapinga na Kerege Wilayani Bagamoyo kujali usalama wao, Usalama wa watumiaji wengine wa barabara na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Ameyasema hayo Septemba 04, 2025 alipofanya kikao na maafisa usafirishaji huko Mapinga ambapo aliwataka kuzingatia sheria za usalama barabarani Kuacha kujihusisha na uhalifu ikiwemo tabia ya kujichukulia sheria mkononi, Kushiriki kubeba mali za wizi bali wawe wepesi kutoa taarifa za uhalifu.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Aziz Zuberi aliwataka maafisa usafirishaji hao kujikagua wao wenyewe kabla hawajaanza safari yaani wahakikishe hawajatumia kilevi na ni wazima kiafya, utimamu wa vyombo vyao vya moto ikiwemo kuwa na leseni ya udereva na chombo kuwa na bima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Maafisa Usafirishaji Wa Mapinga, Kerege na Bagamoyo, Bw Kulwa Msafiri alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Kikosi cha Usalama barabarani kwa namna wanafikisha elimu hiyo mara kwa mara kwa watumiaji wa barabara huku akieleza kuwa imesaidia sana kwani maafisa usafirishaji wa Wilaya hiyo wameacha kabisa tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi inapotokea ajali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad