HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 18, 2025

BARAZA LA USHAURI KWA WATU WENYE ULEMAVU LAPONGEZWA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Mary Maganga amelipongeza Baraza la Ushauri la Taifa kwa Watu wenye Ulemavu kwa mchango mkubwa walioutoa katika kuimarisha haki na ustawi kwa Watu Wenye Ulemavu nchini.

Amesema juhudi hizo zimekuwa chachu ya mafanikio katika kuendeleza ajenda ya usawa, ushirikishwaji na ulinzi wa haki za Watu wenye ulemavu, hatua inayochangia kuimarisha maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi.

Katibu Mkuu Maganga amebainisha hayo leo Septemba 18, 2025 Jijini Dodoma wakati wa kuhitimishwa kwa shughuli za utekelezaji wa baraza hilo kwa kipindi cha Miaka mitatu (2022-2025)

Kuhusu mafanikio yaliyopatikana kupitia baraza hilo Bi.Maganga alitaja ni kukamilika kwa Mwongozo wa Uratibu wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu wa Mwaka 2025, Mkakati wa Taifa wa Teknolojia saidizi wa Mwaka 2024-2027, Mpango wa Taifa wa Haki na Ustawi wa Watu wenye Ualbino, Mwongozo wa Mfuko wa Taifa wa Watu wenye Ulemavu na Mwongozo Taifa wa Viwango vya Ufikivu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt. Lukas Kija ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutoa ruzuku kwa Vyama vya Watu wenye Ulemavu, kutoa vifaa saidizi na kuzindua Mfumo wa kanzi data ya Watu wenye Ulemavu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad