Mhe. Ndejembi amekabidhi hati hiyo kwa Uongozi wa Klabu ya Yanga chini ya Rais wake, Mhandisi Hersi Said katika kilele cha Wiki ya Mwananchi ya Klabu ya Yanga leo Septemba 12, 2025 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“ Siku kadhaa nyuma niliahidi kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu ya Yanga kuwa baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika tutakabidhi hati ya ongezeko la eneo la Klabu hii na leo ninayo furaha kuwatangazia kuwa mchakato umekamilika na nitakabidhi hati hiyo kwa Uongozi wa Timu ya Yanga leo,” Amesema Mhe. Ndejembi.


No comments:
Post a Comment