HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 27, 2025

AfiNet kuzindua “MTOKO” kwa ajili ya kuendeleza wachimbaji wadogo

Katibu wa AfiNet, Edmund Kaiza, amesema shirika hilo linatarajia kuzindua tukio jipya lijulikanalo kama “MTOKO” kupitia programu ya Pop-Up Education for Jobs, itakayofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 17 Oktoba 2025, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa DECA House of Excellence, Mbezi Juu.
Kwa mujibu wa Kaiza, MTOKO inalenga kuendeleza wachimbaji wadogo wa madini kupitia upatikanaji wa teknolojia, utaalamu na rasilimali zinazokidhi mahitaji ya sekta ndogo ya uchimbaji.
Amefafanua kuwa dhumuni kuu la tukio hilo ni kuhusianisha ujuzi na soko la ajira kupitia tafiti na utaalamu elekezi, hususan katika maeneo ya uchimbaji, uchakataji, uchenjuaji, biashara ya madini pamoja na uongezaji thamani.
Kaiza aliongeza kuwa jukwaa hilo litafanyika pia kwa siku tatu katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi, likiwakutanisha wadau wa kimkakati wakiwemo Godtec, NMB Bank Plc na Stamico.

“Kwa kupitia AfiNet, vijana watapata fursa ya kuamsha fikra bunifu na kuzitumia ipasavyo katika kutengeneza nafasi mpya za ajira,” alisema Kaiza.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad