Amuombea kura mgombea Urais CCM Dk.Samia …agusia Katiba Mpya
Na Mwandishi wetu,
MGOMBEA Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Alhaj Abdallah Ulega amewataka watanzania kama wanataka katiba mpya basi wanapaswa kumchagua Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Amesema hata katika uzinduzi wa kampeni kitaifa zilizofanyika jijini Dar es salaam Agost 28,2025 katika Viwanja vya Tanganyika perkas Dk.Samia ametamka kuwa katika siku 100 za mwanzo atahakikisha anafufua upya mchakato wa katiba mpya.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Mkuranga Ulega amesema Dkt .Samia ni muumini wa mariadhiano na akitamka anatenda hivyo watanzania wakiwemo wananchi wa Mkuranga ni kuhakikisha wanampigia kura za kutosha ili aweze kutimiza mambo makubwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi .
.jpeg)
Kuhusu maendeleo yaliyofanyika katika Jimbo la Mkurunga Ulega amesema wananchi hao wakimpa kura za kutosha Dk.Samia pamoja na yeye atakwenda kumuomba Rais kuipandisha hadhi Wilaya ya Mkurunga na kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Mkuranga .
“Wilaya hii inastahili kuwa Manispaa kutokana na uwepo wa viwanda vya kutosha katika Jimbo hilo ambapo amesema hivi sasa wilaya hiyo inaviwanda vidogo zaidi ya 100 na viwanda vikubwa zaidi 70 hivyo inastahili mkuranga kuwa Manispaa.”
Ameongoza kuwa leo umezinduliwa mkutano wa kampeni na yeye na madiwani wake watafanya kampeni za Kistarabu na wanakwenda kata kwa kata ili kumuombea kura Dkt.samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha wanapata kura nyingi.
No comments:
Post a Comment