HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 31, 2025

Wahitimu 50 Bora Sayansi Wapatiwa Ufadhili wa Samia Scholarship Extended

Wahitimu 50 bora wa masomo ya Sayansi katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2025 wamechaguliwa kupata ufadhili kupitia Samia Scholarship Extended, kwa ajili ya kusomea programu za Akili Bandia (Artificial Intelligence), Sayansi ya Data na Sayansi shirikishi nyingine katika vyuo vikuu mahiri duniani.

Akizungumza leo Agosti 31, 2025 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, alisema wahitimu hao wamechaguliwa kutokana na ufaulu wao bora katika masomo ya PCM, PMC na PGM.

Amesema kabla ya kuanza masomo nje ya nchi, vijana hao watawekwa katika Kambi Maalumu ya Maarifa (Boot Camp) kwa kipindi cha miezi 10, ambapo watapewa mafunzo ya msingi ya matumizi ya kompyuta, programu na uchambuzi wa mifumo, sambamba na kusaidiwa katika mchakato wa maombi ya vyuo vikuu vya nje.

“Mafunzo haya yatatolewa na wataalamu wenye ujuzi kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo wataalamu wa sekta binafsi na diaspora, na yatalenga kuwaandaa wanafunzi kupata vyeti vya kitaaluma vinavyotambulika kimataifa,” alieleza Prof. Nombo.

Ufadhili huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, toleo la 2023, inayolenga kutoa elimu bora yenye kuzingatia ujuzi, kulingana na mahitaji ya soko la ajira na stadi za karne ya 21, kwa lengo la kuchangia katika maendeleo ya Taifa na kimataifa.
















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad