HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 4, 2025

TMA Yatoa Elimu Ya Hali Ya Hewa Kwa Wananchi Waliotembelea Maonesho Ya Nanenane

 







MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetumia fursa ya Maonesho Nanenane 2025 kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma kutoa elimu kwa jamii kuhusu huduma zitolewazo na jukumu kubwa la TMA la kudhibiti shughuli za hali ya hewa nchini.

Kupitia maonesho haya, wananchi na wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, wavuvi na wafugaji wamepata elimu ya moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa TMA wakiwemo viongozi.

TMA imeeleza namna taarifa za hali ya hewa zinavyokusanywa, kuchakatwa na kuchambuliwa kupitia mifumo ya kisasa, na jinsi huduma hizo zinavyoweza kusaidia jamii.

Aidha, TMA imeeleza umuhimu wa kuendesha shughuli za hali ya hewa zenye kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), akiwahudumia wateja kwenye banda la mamlaka hiyo aliwahimiza wadau wote kufuatilia utabiri wa kila siku, utabiri wa msimu na tahadhari za hali mbaya ya hewa, huku akisisitiza matumizi sahihi ya taarifa hizo katika shughuli zote za kiuchumi na kijamii.

Ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya hali ya hewa na rasilimali watu na hivyo kuleta maendeleo makubwa ya utendaji kazi wa Mamlaka.

Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania inashiriki katika maonesho ya Nanenane Dodoma, Zanzibar, Mbeya na Morogoro yanayobeba kaulimbiu isemayo “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad