HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 10, 2025

SUKARI BORA YA MKULAZI, YAWAFIKIA WANANCHI KUANZIA UJAZO WA CHINI

Na Mwandishi Wetu

Zaidi ya wakulima 300 kutoka mkoa wa Morogoro wamenufaika na uwepo wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi ambacho kinanunua miwa yao kwa ajili ya uzalishaji wa sukari yenye ubora wa hali ya juu.

Akizungumza katika Maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, Afisa Uhusiano wa Kiwanda hicho, Clementina Patrick, amesema lengo la ushiriki wao katika maonesho hayo si tu kutambulisha bidhaa, bali ni kuwa karibu na wananchi kwa kuwapatia sukari bora inayozalishwa kwa kutumia mitambo ya kisasa.

“Uwepo wa kiwanda hiki umeleta mabadiliko makubwa kwa jamii, wakazi wa maeneo ya jirani, hususan wakulima wa miwa wana uhakika wa soko la mazao yao na hivyo kukuza uchumi wao,” amesema Clementina.

Kwa mujibu wa clementina, Kiwanda cha Mkulazi kinatoa sukari yenye ujazo tofauti tofauti kuanzia kilo moja, kilo 25 na hadi kilo 50, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wananchi wa kipato cha aina yoyote, wanapata bidhaa hiyo muhimu kwa matumizi ya nyumbani na matumizi mengine.

“Wananchi wanakaribishwa kutembelea banda letu Dodoma na Morogoro, tumeweka bei rafiki kwa kila aina ya kipato kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anapata sukari bora ” ameongeza.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad