RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo Agosti 08, 2025 amezindua Maabara ya Rufaa ya Taifa ya Kilimo iliyopo Mtumba Jijini Dodoma.
Maabara hiyo inayosimamiwa na Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inalenga kufanya uchunguzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya Kilimo ili kuongeza tija kwa kufanya utambuzi wa visumbufu vya mimea, afya ya Udongo, utambuzi wa Ubora wa Mbegu na Maabara ya utambuzi viini lishe kwenye mazao.
Aidha, maabara kuu ya Kilimo itashughulika na kupima vimelea vya sumukuvu na sumukuvu yenyewe katika mazao
Akiwa katika uzinduzi huo, Dkt.Samia ameagiza kutafuta eneo kwaajili ya ujenzi wa Ofisi zitakazo kuwa Makao Makuu ya TARI ambazo zitakuwa nje ya eneo hilo la Maabara.
No comments:
Post a Comment