HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 5, 2025

OFISI YA WAKILI MKUU YAENDELEA KUWAKARIBISHA WADAU KWENYE BANDA LAO NANE NANE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika Viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.



Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakisaini kitabu cha wageni wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, wakitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma


Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma
Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Doreen Mhina akitoa maelezo kuhusu masomo ya kuzingatia ili kuwa Wakili wa Serikali kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlangwa walipotembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ndugu Abtwalib Makame akiangalia kipeperushi kinachoelezea majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma
Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Hosana Mgeni akiwapitisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Gabriel kwenye kitabu chenye mkusanyiko wa sheria walipotembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad