HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 8, 2025

MAMLAKA YA AFYA YA MIMEA NA VIUATILIFU YAFUNGUA MASOKO YA NJE KWA WAFANYABAISHARA NCHINI.

Na: Calvin Gwabara - Dodoma

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imewezesha Tanzania kuondolewa vikwazo vya kiubora iliyowekewa kwenye masoko mbalimbali duniani na hivyo kusaidia wakulima wa Tanzania kunufaika na uuzaji wa mazao nje ya nchi.

Mtaalamu wa afya ya mimea kutoka TPHPA Bi. Dorah Amur akifafanua jambo kwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipotembea banda hilo.


Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa afya ya mimea kutoka TPHPA Bi. Dorah Amur wakati akimueleza Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Balozi Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipotembela banda la TPHPA kwenye maonesho ya wakulima nanenane kitaifa Jijini Dodoma kuhusu mafanikio na jitihada zinazofanywa na Taasisi hiyo katika kuhakikisha ubora wa mazao na kufungua masoko.

“Wakulima wa wafanya biashara wa Tanzania wamekuwa wakiuza bidhaa zao kwenye masoko mbalimbali ya kimataifa duniani lakini kuna baadhi ya masoko yalizuia Tanzania kuingiza bidhaa zetu kutokana na sababu mbalimbali za kiubora lakini TPHPA ikaalifanyia kazi haraka kwa kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha kwenye mamlaka za masoko hayo na kufanikiwa kuondolewa kwa zuio hilo na sasa Tanzania inauza bidhaa hzo bila shida” alifafanua Bi. Amuli.

Hata hivyo mtaalamu huyo amesema pamoja na masoko ya mbali lakini pia nchi inanufaika na kuuza mazao kwenye masoko ya afrika mashariki kwani takwimu zinaonesha Tanzania imesafirisha zaidi zao la mchele kwenda kwenye nchi hizo kwa wingi hasa nchini Uganda, ikifuatiwa na Kenya, Rwanda na DRC katika kipindi cha kuanzia mwaka 2024 hadi mwezi mei mwaka 2025.

“Mamla ya Afya ya mimea na viuatilifu Tanzania inajivunia kusaidia wakulima na wafanyabishara wa Tanzania kuyafikia masoko mbalimbali lakini pia kusaidia kuwezesha nchi kunufaika na mauzo ya bidhaa hizo kwa kuhakikisha ubora wa bidhaa zinazosafirishwa na zile zinazoingia kukidhi viwango vya ubora” alieleza Bi. Amuli.

Akizungumzia masuala ya ufungashaji wa bidhaa zinazosafirishwa meneja wa Usimamizi wa afya ya Mimea na karantini kutoka TPHPA bwana Musa Chindinda amesema kuwa hilo ni eneo muhimu ambalo taasisi hiyo inalizingatia na kuhakikisha bidhaa zinazosafirishwa zinakuwa katika hali ya ubora na salama.

“Sio tuu kwamba tunaangalia ubora wa zile zinazosafirishwa lakini pia tunashirikiana na mamlaka zingine kupima na kuhakikisha hata bidhaa zinazoingia nchini zinazingatia ubora hususani vyakula ili kuepusha kuingiza mazao au bidhaa zenye vidudu au magonjwa hatari ambayo yanaweza pelekea kuwekwa kwa karantini” alieleza bwana Chidinda.

Pia amemueleza Mhe. Balozi hatua mbalimbali ambazo zinapaswa kuzingatiwa ili kupata kibali kinachoweza kuruhusu bidhaa hizo kupokelewa na pia kutoa ushauri kwa wafanyabiashara wanaotaka kuuza bidhaa nje ya Tanzania.

Kwa upande wake Balozi huyo wa Tanzania nchini Italia Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amepongeza juhudi hizo kubwa zinazofanywa na TPHPA katika kusaidia kufungua masoko ya bidhaa za Tanzania duniani na kuahidi kuendelea kushirikiana na katika masoko mbalimbali ya mazao nchini Italia.

“Nimefurahi kuona Italia pia bidhaa za Tanzania zinavyopata masoko duniani na kuinua uchumi wa watu na kuingiza nchi fedha za kigeni, Hii sio kazi ndogo hasa kusaidia kuondoa mashaka yanaywekwa na masoko kwa bidhaa za Tanzania kwakweli mnastahili pongezi na niwaombe muendelee kusaidia nchi yetu nami kama balozi nipo tayari kushirikiana nanyi kwenye mambo yoyote ya kimasoko nchini Italia alieleza Mhe. Balozi Mbarouk.

Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu Tanzania inashiriki maonesho ya Kilimo nanenane kitaifa jijini Dodoma na kwenye Kanda zote kupitia ofisi za kanda za Mamlaka hiyo kote nchini.

Meneja wa Usimamizi wa afya ya Mimea na karantini kutoka TPHPA bwana Musa Chindinda akitoa maelezo kwa Balozi.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad