
Roketi hiyo yenye lengo yakufanya maboresho kwenye hali ya hewa.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 49 kimataifa ya sabasaba, mhadhiri mwandamizi chuo kikuu cha UDOM, Dkt. Benatus Mvile amesema Roketi hiyo itasaidia katika maboresho ya mawingu pamoja na mvua kunyesha.
“Tumeshafanya majaribio kadhaa ili kupima kwenda kwenye umbali mkubwa", amesema Dkt Mvile.
Dkt. Mvile ametaja mafanikio ya Roketi hiyo ambayo Taifa italipata ni kwenye shughuli za kilimo ikiwemo kusaidia upatikanaji wa mvua.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo kikuu cha UDOM, Bi. Rose Joseph, amewakaribisha wananchi katika banda la lao ili waweze kupatiwa elimu pamoja na kujionea kazi zinazofanywa na chuo hicho.
“Mwaka huu tumekuna kitofauti mwananchi anapotembelea banda letu atapata elimu juu ya lishe, na tunatoa huduma ya kisheria bure kwa watu wote wenye uhitaji", amesema Bi. Rose Joseph.
Mwisho amesema wamejipanga kutoa elimu namna ya kujiunga na Chuo chao kwa wale wanaohitaji hufuma hiyo maana wamekuja na wataalamu.
No comments:
Post a Comment