HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 4, 2025

MARIET LTD YALETWA BIDHAA MPYA ZA ASILI MAONESHO YA 39 SABASABA

 


KAMPUNI ya Mariet Ltd, wazalishaji maarufu wa bidhaa za Missifiah, imezindua rasmi aina mpya za bidhaa za urembo zinazoenda kuwa suluhisho la matatizo ya ngozi hasa kwa wakina mama na wanawake kwa ujumla.

Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam., Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni hiyo, Frola Julius, amesema kwa mwaka huu Mariet Ltd imewaandalia watumiaji wake bidhaa mbalimbali mpya mbali na zile za awali kama mafuta (oil).

“Mwaka huu tumeleta bidhaa mpya kama body cream, face cream, sabuni za kuogea, toner, serum, shower gel na nyinginezo. Zote ni za asili, zimetengenezwa kwa kutumia mimea ya asili na zinafaa kwa matumizi ya binadamu – wanaume kwa wanawake,” amesema Frola.

Ameongeza kuwa bidhaa hizo zimeidhinishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), jambo linalowapa watumiaji uhakika wa usalama na ubora. “Bidhaa hizi hazina madhara, zinafaa kwa watu wa rika zote, na zina uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali za ngozi kama vile vipele, chunusi na madhara yatokanayo na vipodozi vyenye kemikali kali,” aliongeza.

Frola amewakaribisha wananchi wote wanaotembelea Maonesho ya Sabasaba kufika katika banda la Mariet Ltd ili kujionea na kununua bidhaa hizo zenye uwezo wa kusaidia kurejesha afya ya ngozi kwa njia ya asili.

Mariet Ltd ni mojawapo ya kampuni zinazochipukia kwa kasi katika soko la bidhaa za urembo na afya ya ngozi, na imekuwa ikijizolea sifa kutokana na ubora na matumizi ya malighafi za asili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad