Lengo ni kupata taarifa zitakazosaidia kuandaa MKUMBI II. Utekelezaji wa MKUMBI II unatarajiwa kuongeza kasi katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuleta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali ambazo zitaibuliwa na sekta binafsi.
Aidha, unatarajiwa utachochea uwekezaji wa sekta binafsi kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050 unalenga kuwa na uchumi wa thamani ya Dola Trilioni 1 ifikapo 2050. Huku sekta binafsi ikitarajiwa kuchangia kwa asilimia 65 na kutoa ajira kwa asilimia 85.









No comments:
Post a Comment