*Asisitiza atakuwa na ajenda ya siri na hayuko peke yake,yuko na wenzake
Na Mwandishi Wetu
KADA wa Chama Cha Mapinduzi ambaye amewahi pia kushika nafasi mbalimbali ndani ya Chama hicho Hamis Mgeja ameamua kumtolea uvivu Balozi Humphrey Polepole na kumfananisha na kunguru asiyefugika na ni wa kumuogopa kama ukoma.
Kauli ya Mgeja inakuja baada ya Polepole aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo kwa kutoa madai mbalimbali yakiwemo ya uongozi wa sasa kutokuwa na haki pamoja na uongozi mbovu.
Mgeja ambaye kwa sasa yuko nchini India katika Hospitali ya Nayarana ambako amelazwa kutokana na kusumbuliwa na tatizo la mishipa kutozungusha damu vizuri ametoa taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Julai 15,2025 ambapo ameeleza kutofurahishwa na madai yaliyotolewa na Polepole.
“Ndugu zangu Watanzania kwa sasa nimelazwa hapa nchini India ambako naendelea na matibabu kutokaba na changamoto ya afya lakini nataka mwito wangu kwenu Polepole ni wa kumuogopa kama ukona na nakiomba Chama changu Cha Mapinduzi watu kama aina yakina Polepole sio kuendelea kuwalea.
“Haiwezekani mtu anatoboa boti Mnasafiri naye halafu anatoa maneno ya kinafiki kuwa ataendelea kuwa mwana CCM huo ni unafiki uliobobea.Huyu mwanaharaki na ni sawa na kunguru hafugiki huyu,anataka kurudia kazi yake ya harakati, ni mtu hana shukurani.
“Alipewa uongozi kwa hisani kubwa kuanzia ukatibu mwenezi na sisi makada tulishanga sana maana hakujulikana ametokea wapi.Nadhani Polepole hayuko peke yake ana kundi la hatari lililojificha nyuma yake naomba limulikwe,”amesema Mgeja na kutaja nafasi nyingine alizowahi kupewa Polepole ikiwemo ya Mkuu wa Wilaya na Mjumbe wa Bunge la Katiba lakini matokeo yake amekosa shukrani kwa Serikali.
Mgeja pia anawaomba Watanzania na dunia wampuuze Polepole kwani maneno aliyoyasema ni ya kutafuta njia ya kutokea .”Niwaombe tuendelee kuiunga mkono selikari yetu inayoongozwa na mama yetu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan suluhu kwani tunaona na kushuhudia utawala wa sheria na mihimili yote mitatu inafanyakazi pasipokuingiliana.
“Huo ndio utawala wa sheria uliopo kwetu Tanzania.Unasimamiwa vuzuri kwa weledi mkubwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hasan, kwa hiyo maneno ya Polepole sio bure wala bahati mbaya ,analake jambo na agenda ya siri yeye na wenzake waliojificha.”





No comments:
Post a Comment